Posts

Showing posts from March, 2025

"TOENI RUZUKU KWA JESHI LA MAGEREZA"

Image
Na Paschal D.Lucas Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, ameielekeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutoa ruzuku kwa Jeshi la Magereza ili kuhakikisha magereza yote yanatumia nishati safi ya kupikia. Dkt. Biteko ametoa agizo hilo leo, Machi 28, 2025, jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA). “Magereza yote 129 yamehama kutoka matumizi ya kuni na sasa yanatumia nishati safi ya kupikia. Naielekeza REA kutoa kipaumbele kwa magereza katika ruzuku ya vifaa vya nishati safi,” amesema Dkt. Biteko. Aidha, amewapongeza wahitimu wa mafunzo hayo na kuwataka kuwa chachu ya mabadiliko katika Jeshi la Magereza kwa kusimamia haki, kuwajibisha wazembe, na kuwahamasisha wachapakazi.

BREAKING NEWS:BALOZI JUMA MWAPACHU

Image
  Na Paschal D.Lucas TANZIA: Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kada wa CCM, Balozi Juma Mwapachu amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu. Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi katika mitandao ya kijamii.

MVUA NA UPEPO ZABOMOA NYUMBA NA MIUNDOMBINU MUSOMA

Image
 Mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha usiku wa kuamkia leo, katika mji wa Musoma mkoani Mara imezua na kubomoa nyumba, shule, vituo vya mafuta pamoja nyumba za biashara, baadhi ya majengo ya Airport na miundombinu ya umeme ambapo idadi kamili bado haijafahamika huku ikijeruhi wananchi kadhaa na kusababisha wananchi kukosa makazi na kuharibika kwa mali zao.

ALIYEIBA MAFUTA YA ZAIDI YA MIL 77 MIKONONI MWA POLISI

Image
 Jeshi  la Polisi Mkoani Morogoro limefanikiwa kumkamata Abubakary Mwichangwe (29), Dereva wa lori la mafuta lenye namba za usajili T.661BXW tela namba  T.489 BHC  ambaye alikuwa anatafutwa  Kwa tuhuma za kuiba mafuta aina ya dizeli lita elfu 35 yenye thamani zaidi ya Tsh. milioni 77 kisha kulichoma moto gari hilo kwa lengo kupoteza ushahidi na yeye akatokomea kusikojulikana. Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro SACPnAlex Mkama amesema  tukio hilo limetokea March 16,2025 katika Kijiji cha Msimba Wilaya kilosa Mkoani Morogoro barabara ya Morogoro - Iringa. RPC Mkama amesema Mtuhumiwa aliiba mafuta kwa kula njama na Mameneja wa vituo vya mafuta  kisha alipofika katika Kijiji cha Msimba aliliangusha gari korongoni na kujaribu kulichoma moto kabla ya Wasamaria wema kufika na kuzima na baada ya tukio Dereva alikimbia kusikojulika hadi baadaye Polisi walipomkamata ambapo Polisi haijasema imemkamata akiwa wapi kwasababu za kiupelelezi kwakuwa bado wengine alioku...

ALICHOKISEMA WAZIRI MKUU KWENYE JUBILEI YA MIAKA 25 YA UASKOFU

Image
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema jamii inahitaji kufundishwa, kutambua na kuenzi mila za Kitanzania na kuepuka kuiga tabia za kigeni zisizo na manufaa kwa ustawi wa Taifa. Majaliwa ametoa kauli hiyo leo, Machi 19, 2025, wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Msaidizi Mstaafu wa Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki Bukoba, Askofu Method Kilaini. "Tumeshuhudia ongezeko la vitendo vya ukosefu wa maadili katika jamii. Hali hii inatokana na malezi hafifu na kuiga mila na desturi kutoka mataifa mengine ambazo haziendani na tamaduni na maadili yetu ya Kitanzania," amesema Majaliwa. Waziri Mkuu ameeleza kuwa mabadiliko haya yameathiri hasa vijana, yakiyumbisha misingi ya familia na jamii kwa ujumla. Ameomba Kanisa kuendelea kuwa nguzo ya maadili bora, likitoa mwongozo wa kiroho na kijamii. Pia, ameeleza kutambua mchango wa madhehebu ya dini, ikiwemo Kanisa Katoliki, katika kuboresha ustawi wa jamii na kuahidi ushirikiano wa Serikali katika kulinda na kuimarisha maadili ya K...

ALIYEVUMISHA KUFARIKI KWA RAIS AFIKISHA MAHAKAMANI

Image
 Mwanafunzi wa chuo kikuu nchini Kenya David Oaga Mokaya, anakabiliwa na mashtaka ya kujibu mara baada ya kuchapisha picha ya msafara wa watu wakishiriki msiba wenye nukuu ya kupotosha mtandaoni nchini humo. Ofisi ya mwendesha mashtaka nchini kenya Mokaya anashtakiwa kutumia ukurasa wake wa X zamani twitter, mnamo Novemba 13, 2024, akidai ilikuwa ya mwili wa Rais William Ruto ukiondoka kwenye nyumba ya mazishi ambapo Mahakama imefahamishwa kuwa picha hiyo, iliyoonyesha jeneza lililokuwa limefunikwa bendera ya Kenya na kusindikizwa na maafisa wa kijeshi waliovalia sare za sherehe, ilibuniwa ili kutoa dhana potofu kwamba inamhusisha Rais William Ruto. Bwana Mokaya akiwa mahakamani ametaka kuchunguzwa upya kwa mashtaka yake ambapo kupitia wakili wake Danstan Omari Pamoja na Chama cha Wanasheria nchini Kenya (LSK) wametaka kufahamu endapo Rais William Ruto ataitwa kutoa ushahidi wake. Kesi hiyo sasa imepangwa kusikilizwa kikamilifu Mei 29 mwaka huu kwa ajili ya hatua nyingine za kisher...

KATIBU WA CCM AFARIKI DUNIA

Image
  Na Paschal D.Lucas Taarifa kutokea Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro zinaeleza kuwa katibu wa chama  cha Mapinduzi (CCM )Wilaya ya Rombo Mary Sule amefariki dunia usiku wa Machi 18, 2025 katika Hospitali ya Huruma wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, muda mfupi tu baada ya kutoka kwenye Chumba cha Upasuaji. Marehemu Mary Sule atakumbukwa kwa ujasiri, uchapakazi pamoja na maono na namna alivyokuwa anawashauri viongozi mbalimbali katika wilaya hiyo, kuachana na tabia chonganishi inayodhoofisha maendeleo, huku akiwasisitiza viongozi kufuata Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi. Kwa taarifa zaidi tutawalete.....

TAARIFA RASMI JUU YA KUANGUKA KWA NDEGE DAR

Image
 Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imetolea ufafanuzi zoezi la utayari walilolifanya na kuonesha kuwa ndege ilianguka katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.  Taarifa yao waliyoandika katika ukurasa lao rasmi wa Instagram mara baada ya kutokea kwa taharuki hiyo imesomeka hivi: Taharuki imetokea leo katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kutokana na kusambaa kwa taarifa za kutokea kwa ajali ya ndege aina ya Boeing 787-9 iliyokuwa ikitokea Lanseria Afrika ya Kusini majira ya saa 1.55 asubuhi ikiwa na abiria 139 pamoja na wahudumu wa ndege. Katika ajali hiyo kulikuwa na majeruhi na abiria waliofariki 9 ikiwa taarifa za ajali hiyo iliyotokana na shambulio la ndege hai lililopelekea hitilafu katika injini na kusababisha kuanguka kwa ndege kuwaka moto.  Maofisa kutoka vyombo mbalimbali vya dola wakiwemo Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji, taasisi za Serikali zikiwemo Hospitali, Shirika la Msalaba...

HII NDIYO PICHA YA PAPA TANGU ALAZWE

Image
  Na Paschal D.Lucas Vatican imetoa picha ya kwanza ya Papa Francis tangu alipolazwa hospitalini mwezi mmoja uliopita. Picha hiyo inamuonyesha Papa akiwa amekaa kwenye kiti cha magurudumu mbele ya madhabahu kwenye kanisa moja katika Hospitali ya Gemelli ya Rome, ambako amekuwa akipata nafuu kutokana na nimonia. Mapema Jumapili, katika ujumbe wake, Papa alisema amepitia “kipindi cha majaribio” alipokuwa akiwashukuru watu wanaomtakia mema kwa maombi yao, na kuombea amani katika "nchi zilizoathirika na vita". Aliadhimisha Jumapili ya tano mfululizo ambayo Papa hakuhudhuria Kanisani. Vatican ilisema mapema wiki hii kwamba X-ray ilithibitisha "kuimarika" kwa afya yake, lakini bado anahitaji matibabu ya hospitali.

JESCA MAGUFULI AONGOZA MAANDAMANO

Image
  Taarifa iliyotolewa na AYO TV Familia ya Hayati Rais John Pombe Magufuli ikiongozwa na Mtoto wa Dr. Magufuli aitwaye Jesca Magufuli, imeongoza maandamano ya amani leo March 16 2025 Chato, Geita kumuenzi Hayati Magufuli na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza na kukamilisha miradi iliyoanzishwa na Hayati Magufuli. Maandamano hayo ambayo Mgeni rasmi wake alikuwa ni Rehema Sombi Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa (UVCCM) yalifika hadi Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato kutoa msaada kwa Wanawake waliojifungua pamoja na wale Wajawazito na kuchangia damu. Matembezi hayo yaliongoza mamia ya Vijana yalikwenda pia mpaka kwenye kaburi la Hayati Magufuli lililopo nyumbani kwake Chato ambapo wamefanya Ibada ya kumuombea Hayati Magufuli, ibada ambayo pia imehudhuriwa na Viongozi wengine wa UVCCM kutoka Mtwara, Arusha, Kigoma na Geita. Dr. John Pombe Magufuli ambaye alizaliwa October 29, 1959 alifariki dunia March 17,2021 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es s...

TRUMP AKIFUNGIA KITUO HIKI CHA HABARI

Image
  Habari za Tovuti na Paschal D.Lucas Rais wa Marekani Donald Trump wa ameamuru kufungwa kwa muda Kituo cha Habari cha Sauti ya Amerika (VOA), hatua iliyosababisha zaidi ya wafanyakazi 1,300 kuwa kwenye likizo ya lazima.  Uamuzi wa Trump umeyaathiri pia mashirika sita ya habari yanayofadhiliwa na Serikali ya shirikisho ikiwa ni pamoja na Redio Free Europe na Redio Free Asia. Mkurugenzi wa VOA  Kituo cha habari hicho ambacho hutangaza kwa karibu lugha 50, Michael Abramowitz ameeleza kusikitishwa na uamuzi huo, akisema hii ni mara ya kwanza baada ya miaka 83 Sauti ya Amerika inazimwa.  Amesema VOA imekuwa na jukumu muhimu katika kupigania uhuru na demokrasia kote duniani, na kwamba uamuzi wa Trump unakiathiri chombo hicho ambacho hutumika kama chanzo cha habari za kuaminika katika mataifa mbalimbali.  Shirika la kimataifa la waandishi wa habari wasiokuwa na mipaka limelaani uamuzi huo wa Rais Trump na kulitaka Bunge la Marekani na Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hat...

"Tuma kwa Namba Hii" MIKONONI MWA POLISI

Image
  Na Paschal D.Lucas,(Geita) Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kukutwa na laini za simu 9,389 za mitandao mbalimbali ya simu, ambazo walikuwa wakizitumia kufanyia uhalifu kwa njia ya mtandao na unyang'anyi. Watuhumiwa hao pia wamekutwa na vifaa mbalimbali vya kufanyia uhalifu ikiwemo kompyuta mpakato, mashine mbili za kusajili laini kwa kutumia alama za vidole, simu janja 15 na simu ndogo za kawaida 18.   Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Safia Jongo imeeleza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa Machi 13, 2025 katika Kata ya Ludete wilayani Geita ambapo Jeshi la Polisi lilipata taarifa juu ya uwepo wa wahalifu hao na kuweka mtego uliofanikisha kuwakamata wakiwa na vifaa vya kufanyia uhalifu. Jeshi la Polisi mkoani Geita linaendelea na uchunguzi kwa kushirikiana na taasisi nyingine ili kuweza kubaini mtandao mzima wa wahalifu hao na kuwachukulia hatua za kisheria.

MARUFUKU KUINGIA MAREKANI

Image
Kutoka Mtandaoni na Paschal D.Lucas Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Dw limesema kuwa utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump umetoa pendekezo la kuweka marufuku mpya ya kusafiri kuingia nchini humo itakayowaathiri Raia wa Mataifa kadhaa kwa viwango vinavyotofautiana. Kwa mujibu wa gazeti la Marekani la New York Times lililowanukuu Maafisa ambao hawakutajwa majina limesema pendekezo hilo linazihusisha nchi 43. Miongoni mwa nchi hizo ambazo Raia wake watazuiwa kabisa kuingia Marekani ni Afghanistan, Libya, Korea Kaskazini, Somalia, Sudan, Syria, Venezuela na Yemen, kundi jingine ni la nchi nyingine kumi zikiwemo Belarus, Eritrea, Haiti,  Pakistan, Russia  Sierra Leone na Sudan Kusini ambazo visa zao zitawekewa vikwazo vikali. Nchi nyingine 22 zitapewa siku 60 za kushughulikia masuala yanayoipa wasiwasi wa Marekani vinginevyo zitahamishiwa kwenye makundi yaliyowekewa vizingizi vikali zaidi.  Itakumbukwa pia kuwa katika muhula wake wa kwanza wa uongozi, Rais wa Marekani D...

SGR NDANI YA BURUNDI

Image
Na Paschal D.Lucas (Tabora) Katika kuendeleza na kutekeleza mradi wa ujenzi wa reli ya mwendokasi(SGR) zaidi ya shilingi trilioni moja imetolewa na Serikali kutekeleza mradi wa  reli ya kisasa  SGR LOT NO 6 ya kutoka Tabora kwenda mkoani Kigoma mpaka Msongati nchini Burundi mradi ambao kwa sasa uko katika hatua za awali ukiwa umefika asilimia 7.  Akizungumza na waandishi wa habari mkoani kigoma, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PIC), Mh. Augustine Holle amesema fedha za utekelezaji wa mradi huo ni makusanyo ya fedha za Serikali na kuongezea kuwa mradi huu ni sehemu ya mpango wa kuimarisha miundombinu ya reli nchini ili kurahisisha usafiri wa mizigo kati ya mikoa hiyo na nchi jirani za Burundi na Congo.

NYASAKA AJIUA NA KUACHA UJUMBE MZITO

Image
Na Paschal D.Lucas, Mara. Habari kutokea nchini Kenya zinaeleza kuwa Mwanamke aliyetambulika kama Mercy Nyasaka amejiua baada ya kuacha ujumbe mzito kwa ndugu wa karibu kupitia Whatsapp akimuaga na kueleza anayoyapitia. Mercy alifiwa na bintiye miaka miwili iliyopita mnamo Machi 1, 2023, kifo ambacho kilimsababishia huzuni kwa kiasi kikubwa kulingana na machapisho yake mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii hasa Facebook. Licha ya kufiwa na bintiye Mercy, mara kadhaa alichapisha machapisho yaliyoashiria kuhisi kukatishwa tamaa na mwenzi wake, na misukosuko mingine ya maisha ikiwemo na matatizo ya kifedha. Katika ujumbe aliotuma siku ya Ijumaa kupitia WhatsApp kwa ndugu yake wa karibu, Mercy alimfahamisha kwamba hawezi kuendelea kuyakabili matatizo ya maisha pamoja na kifo cha bintiye, ikiwa ni pamoja na mkopo wa gari.   "Samahani kwa kukukatisha tamaa kwa njia hii lakini wakati utapata ujumbe huu nitakuwa nimeondoka kwa muda mrefu," sehemu ya ujumbe aliotuma Mercy.

KUFURU YA SINGIDA BLACK STARS KUZINDUA UWANJA HUU

Image
  Na Paschal D.Lucas (Mwanza) Klabu ya Singida Black Stars imetangaza rasmi uzinduzi wa uwanja wao mpya wa kisasa unaoitwa Airtel Stadium, uliopo katika eneo la Mtipa, mkoani Singida. Uzinduzi wa uwanja huo mpya wa klabu hiyo utafanyika Machi 24, 2025, mkoani Singida, ambapo watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Wananchi, Yanga SC. "Airtel Stadium ni sehemu ya dhamira ya Singida Black Stars ya kuwekeza katika maendeleo ya michezo kwa kutoa mazingira bora kwa wachezaji, mashabiki, na jamii kwa ujumla. Uwanja huu umejengwa kwa viwango vya kimataifa na unatarajiwa kuwa kitovu cha mashindano makubwa ya kitaifa na kimataifa," imeeleza taarifa ya klabu hiyo.

Breaking News: Blog ya Paschal D.Lucas (Informer) Iko hewani kuanzia sasa.

Image
Baada ya kipindi cha miaka mitano kutokuwa hewani kwa ukurasa wa habari wa Paschal D.Lucas, Habari njema kuanzia sasa imerudi hewani. Karibuni kuweza kupata taarifa mbalimbali zote zikiwemo za Siasa, Dini, Burudani na Michezo kutoka ndani na nje ya nchi. Habari kuhusu Jamii na Mafunzo pia kupitia teknolojia mbalimbali na kazi zinazofanyika katika jamii kwa ujumla. Pia kwa Upande wa Mitandao yote ya kijamii ( Facebook, Instagram, X zamani Twitter,Thread) tunapatika kwa jina hilo hilo la Paschal D Lucas. Kwa upande wa Online Tv kwa maana ya Youtube tunaoatikana kwa jina la DLucasDigital . Karibuni sana sana!