NYASAKA AJIUA NA KUACHA UJUMBE MZITO



Na Paschal D.Lucas, Mara.

Habari kutokea nchini Kenya zinaeleza kuwa Mwanamke aliyetambulika kama Mercy Nyasaka amejiua baada ya kuacha ujumbe mzito kwa ndugu wa karibu kupitia Whatsapp akimuaga na kueleza anayoyapitia. Mercy alifiwa na bintiye miaka miwili iliyopita mnamo Machi 1, 2023, kifo ambacho kilimsababishia huzuni kwa kiasi kikubwa kulingana na machapisho yake mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii hasa Facebook.


Licha ya kufiwa na bintiye Mercy, mara kadhaa alichapisha machapisho yaliyoashiria kuhisi kukatishwa tamaa na mwenzi wake, na misukosuko mingine ya maisha ikiwemo na matatizo ya kifedha.


Katika ujumbe aliotuma siku ya Ijumaa kupitia WhatsApp kwa ndugu yake wa karibu, Mercy alimfahamisha kwamba hawezi kuendelea kuyakabili matatizo ya maisha pamoja na kifo cha bintiye, ikiwa ni pamoja na mkopo wa gari.

 


"Samahani kwa kukukatisha tamaa kwa njia hii lakini wakati utapata ujumbe huu nitakuwa nimeondoka kwa muda mrefu," sehemu ya ujumbe aliotuma Mercy.

Comments

Popular posts from this blog

BREAKING NEWS: MKURUGENZI WA TANESCO AFARIKI BUNDA KWA AJALI

MIAKA 30 JELA NGUNO WA KWIMBA KWA KUMBAKA KIZIWI

TANZANIA YAISHUKURU ITALIA KUHUSU SGR