SGR NDANI YA BURUNDI


Na Paschal D.Lucas (Tabora)

Katika kuendeleza na kutekeleza mradi wa ujenzi wa reli ya mwendokasi(SGR) zaidi ya shilingi trilioni moja imetolewa na Serikali kutekeleza mradi wa  reli ya kisasa  SGR LOT NO 6 ya kutoka Tabora kwenda mkoani Kigoma mpaka Msongati nchini Burundi mradi ambao kwa sasa uko katika hatua za awali ukiwa umefika asilimia 7. 


Akizungumza na waandishi wa habari mkoani kigoma, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PIC), Mh. Augustine Holle amesema fedha za utekelezaji wa mradi huo ni makusanyo ya fedha za Serikali na kuongezea kuwa mradi huu ni sehemu ya mpango wa kuimarisha miundombinu ya reli nchini ili kurahisisha usafiri wa mizigo kati ya mikoa hiyo na nchi jirani za Burundi na Congo.

Comments

Popular posts from this blog

BREAKING NEWS: MKURUGENZI WA TANESCO AFARIKI BUNDA KWA AJALI

MIAKA 30 JELA NGUNO WA KWIMBA KWA KUMBAKA KIZIWI

TANZANIA YAISHUKURU ITALIA KUHUSU SGR