KATIBU WA CCM AFARIKI DUNIA
Na Paschal D.Lucas
Taarifa kutokea Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro zinaeleza kuwa katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM )Wilaya ya Rombo Mary Sule amefariki dunia usiku wa Machi 18, 2025 katika Hospitali ya Huruma wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, muda mfupi tu baada ya kutoka kwenye Chumba cha Upasuaji.
Marehemu Mary Sule atakumbukwa kwa ujasiri, uchapakazi pamoja na maono na namna alivyokuwa anawashauri viongozi mbalimbali katika wilaya hiyo, kuachana na tabia chonganishi inayodhoofisha maendeleo, huku akiwasisitiza viongozi kufuata Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
Kwa taarifa zaidi tutawalete.....

Comments
Post a Comment