TAARIFA RASMI JUU YA KUANGUKA KWA NDEGE DAR
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imetolea ufafanuzi zoezi la utayari walilolifanya na kuonesha kuwa ndege ilianguka katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Taarifa yao waliyoandika katika ukurasa lao rasmi wa Instagram mara baada ya kutokea kwa taharuki hiyo imesomeka hivi:
Taharuki imetokea leo katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kutokana na kusambaa kwa taarifa za kutokea kwa ajali ya ndege aina ya Boeing 787-9 iliyokuwa ikitokea Lanseria Afrika ya Kusini majira ya saa 1.55 asubuhi ikiwa na abiria 139 pamoja na wahudumu wa ndege.
Katika ajali hiyo kulikuwa na majeruhi na abiria waliofariki 9 ikiwa taarifa za ajali hiyo iliyotokana na shambulio la ndege hai lililopelekea hitilafu katika injini na kusababisha kuanguka kwa ndege kuwaka moto.
Maofisa kutoka vyombo mbalimbali vya dola wakiwemo Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji, taasisi za Serikali zikiwemo Hospitali, Shirika la Msalaba Mwekundu pamoja na Wadau mbalimbali wa Kiwanja waliweza kufika mara moja eneo la tukio kwa ajili ya uokozi huku baadhi ya abiria walipoteza fahamu, majeruhi waliweza kupata msaada wa haraka kwa kupatiwa huduma ya kwanza na kupelekwa hospitali mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Kamishna Msaidizi na Kaimu Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege Tanzania, Said Ramadhani Kitanto amesema hilo lilikuwa zoezi maalum la utayari kuona kiwanja cha JNIA kiko tayari kiasi gani katika kukabiliana na majanga na dharura.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa kiwanja hicho Bi. Bertha Bakwa amesema, zoezi hilo ni juhudi za kuimarisha usalama kwa kukabiliana na majanga na limefanyika kwa mujibu wa taratibu na miongozo ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) pamoja na miongozo ya Shirika la Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Pia ameendelea kusema kuwa ikumbukwe kiwanja cha JNIA ni kinara katika Viwanja Afrika kwani kiliweza kupata tuzo ya Usalama iliyotolewa na Baraza la Viwanja vya Ndege Afrika (ACI) Septemba, 2024 hivyo ni wajibu wa Kiwanja kuonyesha kilichopatikana kinathibitishwa kwa umma kwa kuendelea kukifanyia majaribio

Comments
Post a Comment