MARUFUKU KUINGIA MAREKANI

Kutoka Mtandaoni na Paschal D.Lucas


Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Dw limesema kuwa utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump umetoa pendekezo la kuweka marufuku mpya ya kusafiri kuingia nchini humo itakayowaathiri Raia wa Mataifa kadhaa kwa viwango vinavyotofautiana.


Kwa mujibu wa gazeti la Marekani la New York Times lililowanukuu Maafisa ambao hawakutajwa majina limesema pendekezo hilo linazihusisha nchi 43.


Miongoni mwa nchi hizo ambazo Raia wake watazuiwa kabisa kuingia Marekani ni Afghanistan, Libya, Korea Kaskazini, Somalia, Sudan, Syria, Venezuela na Yemen, kundi jingine ni la nchi nyingine kumi zikiwemo Belarus, Eritrea, Haiti,  Pakistan, Russia  Sierra Leone na Sudan Kusini ambazo visa zao zitawekewa vikwazo vikali.


Nchi nyingine 22 zitapewa siku 60 za kushughulikia masuala yanayoipa wasiwasi wa Marekani vinginevyo zitahamishiwa kwenye makundi yaliyowekewa vizingizi vikali zaidi. 


Itakumbukwa pia kuwa katika muhula wake wa kwanza wa uongozi, Rais wa Marekani Donald Trump aliiamuru Serikali kuainisha nchi ambazo Raia wake hawapaswi kuingia nchini mwake kwa sababu za kiusalama.

Comments

Popular posts from this blog

BREAKING NEWS: MKURUGENZI WA TANESCO AFARIKI BUNDA KWA AJALI

MIAKA 30 JELA NGUNO WA KWIMBA KWA KUMBAKA KIZIWI

TANZANIA YAISHUKURU ITALIA KUHUSU SGR