ALIYEVUMISHA KUFARIKI KWA RAIS AFIKISHA MAHAKAMANI


 Mwanafunzi wa chuo kikuu nchini Kenya David Oaga Mokaya, anakabiliwa na mashtaka ya kujibu mara baada ya kuchapisha picha ya msafara wa watu wakishiriki msiba wenye nukuu ya kupotosha mtandaoni nchini humo.

Ofisi ya mwendesha mashtaka nchini kenya Mokaya anashtakiwa kutumia ukurasa wake wa X zamani twitter, mnamo Novemba 13, 2024, akidai ilikuwa ya mwili wa Rais William Ruto ukiondoka kwenye nyumba ya mazishi ambapo Mahakama imefahamishwa kuwa picha hiyo, iliyoonyesha jeneza lililokuwa limefunikwa bendera ya Kenya na kusindikizwa na maafisa wa kijeshi waliovalia sare za sherehe, ilibuniwa ili kutoa dhana potofu kwamba inamhusisha Rais William Ruto.


Bwana Mokaya akiwa mahakamani ametaka kuchunguzwa upya kwa mashtaka yake ambapo kupitia wakili wake Danstan Omari Pamoja na Chama cha Wanasheria nchini Kenya (LSK) wametaka kufahamu endapo Rais William Ruto ataitwa kutoa ushahidi wake. Kesi hiyo sasa imepangwa kusikilizwa kikamilifu Mei 29 mwaka huu kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.

Comments

Popular posts from this blog

BREAKING NEWS: MKURUGENZI WA TANESCO AFARIKI BUNDA KWA AJALI

MIAKA 30 JELA NGUNO WA KWIMBA KWA KUMBAKA KIZIWI

TANZANIA YAISHUKURU ITALIA KUHUSU SGR