HII NDIYO PICHA YA PAPA TANGU ALAZWE
Na Paschal D.Lucas
Vatican imetoa picha ya kwanza ya Papa Francis tangu alipolazwa hospitalini mwezi mmoja uliopita.
Picha hiyo inamuonyesha Papa akiwa amekaa kwenye kiti cha magurudumu mbele ya madhabahu kwenye kanisa moja katika Hospitali ya Gemelli ya Rome, ambako amekuwa akipata nafuu kutokana na nimonia.
Mapema Jumapili, katika ujumbe wake, Papa alisema amepitia “kipindi cha majaribio” alipokuwa akiwashukuru watu wanaomtakia mema kwa maombi yao, na kuombea amani katika "nchi zilizoathirika na vita".
Aliadhimisha Jumapili ya tano mfululizo ambayo Papa hakuhudhuria Kanisani. Vatican ilisema mapema wiki hii kwamba X-ray ilithibitisha "kuimarika" kwa afya yake, lakini bado anahitaji matibabu ya hospitali.

Comments
Post a Comment