"TOENI RUZUKU KWA JESHI LA MAGEREZA"

Na Paschal D.Lucas

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, ameielekeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutoa ruzuku kwa Jeshi la Magereza ili kuhakikisha magereza yote yanatumia nishati safi ya kupikia.


Dkt. Biteko ametoa agizo hilo leo, Machi 28, 2025, jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA).


“Magereza yote 129 yamehama kutoka matumizi ya kuni na sasa yanatumia nishati safi ya kupikia. Naielekeza REA kutoa kipaumbele kwa magereza katika ruzuku ya vifaa vya nishati safi,” amesema Dkt. Biteko.


Aidha, amewapongeza wahitimu wa mafunzo hayo na kuwataka kuwa chachu ya mabadiliko katika Jeshi la Magereza kwa kusimamia haki, kuwajibisha wazembe, na kuwahamasisha wachapakazi.

Comments

Popular posts from this blog

BREAKING NEWS: MKURUGENZI WA TANESCO AFARIKI BUNDA KWA AJALI

MIAKA 30 JELA NGUNO WA KWIMBA KWA KUMBAKA KIZIWI

TANZANIA YAISHUKURU ITALIA KUHUSU SGR