JESCA MAGUFULI AONGOZA MAANDAMANO

 

Taarifa iliyotolewa na AYO TV

Familia ya Hayati Rais John Pombe Magufuli ikiongozwa na Mtoto wa Dr. Magufuli aitwaye Jesca Magufuli, imeongoza maandamano ya amani leo March 16 2025 Chato, Geita kumuenzi Hayati Magufuli na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza na kukamilisha miradi iliyoanzishwa na Hayati Magufuli.


Maandamano hayo ambayo Mgeni rasmi wake alikuwa ni Rehema Sombi Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa (UVCCM) yalifika hadi Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato kutoa msaada kwa Wanawake waliojifungua pamoja na wale Wajawazito na kuchangia damu.


Matembezi hayo yaliongoza mamia ya Vijana yalikwenda pia mpaka kwenye kaburi la Hayati Magufuli lililopo nyumbani kwake Chato ambapo wamefanya Ibada ya kumuombea Hayati Magufuli, ibada ambayo pia imehudhuriwa na Viongozi wengine wa UVCCM kutoka Mtwara, Arusha, Kigoma na Geita.


Dr. John Pombe Magufuli ambaye alizaliwa October 29, 1959 alifariki dunia March 17,2021 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ambapo alizikwa kwenye makaburi ya Familia nyumbani kwake Chato ljumaa March 26,2021.

NB.Picha na Habari ni kwa Mujibu wa Ayo Tv


Comments

Popular posts from this blog

BREAKING NEWS: MKURUGENZI WA TANESCO AFARIKI BUNDA KWA AJALI

MIAKA 30 JELA NGUNO WA KWIMBA KWA KUMBAKA KIZIWI

TANZANIA YAISHUKURU ITALIA KUHUSU SGR