Posts

TEC YALAANI KUSHAMBULIWA KWA PADRE KITIMA

Image
Waraka wa Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania (TEC) umesema Padre Kitima alipata majeraha makubwa na kuwa amelazwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam. Katika waraka wake, TEC imelitaka jeshi la polisi na vyombo vingine kuchukua hatua za haraka kuwabaini na kuwakamata wale wote waliohusika katika kupanga na kutekeleza uhalifu huo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. ''Uchunguzi wa tukio hilo ufayike haraka na taarifa zitolewe kwa uwazi bila upotoshaji wowote ili kurudisha imani na matumaini kwa watu wetu''. Ilisema sehemu ya waraka huo.

UNDANI KUHUSU KIFO CHA PAPA FRANSIC

Image
Na Paschal D.Lucas ( Kutoka kwenye Tovuti ) Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amefariki dunia Jumatatu ya Pasaka, Aprili 21, 2025, akiwa na umri wa miaka 88 katika makazi yake katika Casa Santa Marta, Vatican. Muda mfupi uliopita, Mwadhama, Kardinali Farrell, alitangaza kwa masikitiko kifo cha Baba Mtakatifu Francis. Kifo cha Papa kimekuja chini ya saa 24 baada ya kujitokeza kwenye Uwanja wa St Peter's Square mjini Vatican kwa ajili ya Jumapili ya Pasaka. Alitoka akiwa kwenye kiti cha magurudumu na kupunga mkono kutoka kwenye baraza ya Basilica ya St Peter's kwa umati wa watu waliokuwa wakishangilia na kusema: "Ndugu wapendwa, Pasaka njema." Hotuba yake ya Pasaka na baraka ilisomwa na msaidizi alipokuwa ameketi, akitazama. Baada ya baraka, alizungushwa kwenye uwanja. Alipopita katikati ya umati, msafara wake ulisimama mara kadhaa huku watoto wachanga wakiletwa ili awabariki. Katika miezi ya mwisho ya maisha yake, hali mbaya ya afya ya Papa ilimfanya ku...

BREAKING NEWS: MKURUGENZI WA TANESCO AFARIKI BUNDA KWA AJALI

Image
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga amefariki dunia kwenye ajali ya gari iliyotokea wilayani  Bunda Mkoa wa Mara. Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mara, Nickson Babu amethibitisha taarifa hizo ambapo amesema Nyamo-Hanga amefariki dunia pamoja na dereva wake. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda. 

VYAMA VILIVYORIDHIA NA KUSAINI KANUNI ZA MAADILI YA UCHAGUZI

Image
Vyama vipatavyo 18 vya Siasa vimeridhia kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa mwaka 2025, hivyo kupata sifa ya kushiriki kwenye uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu Pamoja na chaguzi nyingine zote ndogo zitakazofanyika ndani ya miaka mitano ijayo. Haya yamebainishwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhan Kailima, na kwamba vyama vya siasa 18 kati ya 19 ndivyo vimesaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi 2025 na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hakijasaini.    "Maadili ya uchaguzi ni muhimu katika kuwezesha uchaguzi huru na haki, na ni muhimu kwa pande zote kuhusika na kusaini maadili hayo, mchakato wa maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani" Amesema Kailima.  Vyama 18 vilivyoridhia kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi 2025, ni  ACT WAZALENDO, AAFP,ADA-TADEA, ADC, CCK, CCM, CHAUMA, CUF, MAKINI, DP, NCCR-Mageuzi, NLD, NRA, SAU, TLP, UDP,  UPDP na UMD.

MAAMUZI YA WAASI WA M23 LEO NCHINI QATAR

Image
 Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kundi la waasi la M23 wanatazamiwa kufanya mazungumzo yao ya kwanza ya moja kwa moja leo Tarehe 09 Aprili, 2025 mjini Doha nchini Qatar. Hii inaonesha hatua iliyopigwa kuelekea juhudi za kumaliza moja ya migogoro mikali zaidi katika Afrika ya Kati. Siku moja baada ya M23 kujiondoa kwa mazungumzo ya amani, Tarehe 18 mwezi Machi Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Felix Tshisekedi, na Paul Kagame Rais wa Rwanda, walikutana nchini Qatar kwa mazungumzo yao ya kwanza ya ana kwa ana mpatanishi mkuu akiwa ni Amir wa Qatar. Haya yanajiri baada ya Angola kujiondoa kama mpatanishi mkuu wa mzozo kati ya Kongo na M23. Mzozo wa mashariki mwa Kongo umedumu kwa muda sasa, madini yakitajwa kama kichochea kikubwa, Mzozo umeongezeka haraka tangu Januari 2025, na Maelfu ya watu waliuawa na mamia wakalazimika kuyakimbia makazi yao.

WATU 80 WAMEFARIKI NA WENGINE 150 WAMEJERUHIWA BAADA YA PAA KUANGUKA

Image
 Maafisa wa uokozi katika Jamhuri ya Dominican wanasema watu takriban themanini wamefariki dunia na 150 kujeruhiwa baada ya paa la ukumbi wa burudani kuanguka wakati wa tamasha la msanii Rubby Perez. Msanii huyo ni miongoni mwa hao waliofariki dunia. Maafisa hao wa uokozi wanawatafuta manusura katika ukumbi huo ulioko mji mkuu Santo Domingo uliojengwa miaka ya sabini iliyopita. Mkurugenzi wa Kituo cha Operesheni za Dharura (COE), Juan Manuel Méndez, alisema ana matumaini kwamba wengi wa waliozikwa chini ya paa lililoporomoka bado wako hai. Jet Set ni klabu ya usiku maarufu huko Santo Domingo ambayo huandaa mara kwa mara matamasha ya muziki wa dansi Jumatatu jioni. Wanasiasa, wanamichezo na watu wengine mashuhuri walihudhuria. Kwa mujibu wa Gavana wa Jimbo la Monte Cristi Rais Luis Abinader  amesema miongoni mwa waathirika ni Nelsy Cruz.

MIAKA 30 JELA NGUNO WA KWIMBA KWA KUMBAKA KIZIWI

Image
  Na Paschal D.Lucas,Mwanza Kutoka Mahakama ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza imemhukumu Malimo Mathias Nguno kwa jina maarufu Gohe (41), kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumkuta na hatia ya kumbaka mtoto (13) mwenye ulemavu wa kusikia (kiziwi). Hukumu hiyo imesomwa leo Aprili 08, 2025 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Ndeko Dastan Ndeko. Kwa mujibu wa hakimu Ndeko, mshtakiwa alitenda kosa hilo katika kesi hiyo ya jinai namba 2904/2025  kinyume na vifungu namba 130(1)(2)(e) na 131(1) vya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022. “Baada ya kupitia vifungu vya sheria na kujiridhisha na ushahidi uliowasilishwa na upande wa Jamhuri ambao haukuacha shaka lolote na hivyo mahakama hii imekukuta na hatia ya kumbaka kigori (13) (jina limehifadhiwa),” amesema Hakimu huyo. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshatakiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 04.01.2025, katika Kijiji cha Nyambuyi kilichopo ndani ya wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza kwa mwathiriwa ambaye ana ulemavu wa kus...