WATU 80 WAMEFARIKI NA WENGINE 150 WAMEJERUHIWA BAADA YA PAA KUANGUKA


 Maafisa wa uokozi katika Jamhuri ya Dominican wanasema watu takriban themanini wamefariki dunia na 150 kujeruhiwa baada ya paa la ukumbi wa burudani kuanguka wakati wa tamasha la msanii Rubby Perez.


Msanii huyo ni miongoni mwa hao waliofariki dunia.


Maafisa hao wa uokozi wanawatafuta manusura katika ukumbi huo ulioko mji mkuu Santo Domingo uliojengwa miaka ya sabini iliyopita.


Mkurugenzi wa Kituo cha Operesheni za Dharura (COE), Juan Manuel Méndez, alisema ana matumaini kwamba wengi wa waliozikwa chini ya paa lililoporomoka bado wako hai.


Jet Set ni klabu ya usiku maarufu huko Santo Domingo ambayo huandaa mara kwa mara matamasha ya muziki wa dansi Jumatatu jioni.


Wanasiasa, wanamichezo na watu wengine mashuhuri walihudhuria.


Kwa mujibu wa Gavana wa Jimbo la Monte Cristi Rais Luis Abinader  amesema miongoni mwa waathirika ni Nelsy Cruz.


Comments

Popular posts from this blog

BREAKING NEWS: MKURUGENZI WA TANESCO AFARIKI BUNDA KWA AJALI

MIAKA 30 JELA NGUNO WA KWIMBA KWA KUMBAKA KIZIWI

TANZANIA YAISHUKURU ITALIA KUHUSU SGR