UNDANI KUHUSU KIFO CHA PAPA FRANSIC


Na Paschal D.Lucas (Kutoka kwenye Tovuti)

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amefariki dunia Jumatatu ya Pasaka, Aprili 21, 2025, akiwa na umri wa miaka 88 katika makazi yake katika Casa Santa Marta, Vatican.

Muda mfupi uliopita, Mwadhama, Kardinali Farrell, alitangaza kwa masikitiko kifo cha Baba Mtakatifu Francis.

Kifo cha Papa kimekuja chini ya saa 24 baada ya kujitokeza kwenye Uwanja wa St Peter's Square mjini Vatican kwa ajili ya Jumapili ya Pasaka.

Alitoka akiwa kwenye kiti cha magurudumu na kupunga mkono kutoka kwenye baraza ya Basilica ya St Peter's kwa umati wa watu waliokuwa wakishangilia na kusema: "Ndugu wapendwa, Pasaka njema."

Hotuba yake ya Pasaka na baraka ilisomwa na msaidizi alipokuwa ameketi, akitazama.

Baada ya baraka, alizungushwa kwenye uwanja. Alipopita katikati ya umati, msafara wake ulisimama mara kadhaa huku watoto wachanga wakiletwa ili awabariki.

Katika miezi ya mwisho ya maisha yake, hali mbaya ya afya ya Papa ilimfanya kutumia wiki kadhaa hospitalini.

Mnamo tarehe 14 Februari, Papa akiwa na miaka 88 alipelekwa katika hospitali ya Gemelli huko Roma kutibiwa homa ya mapafu. Alikuwa na shida ya kupumua kwa siku kadhaa ambapo aliruhusiwa kutoka hospitali mnamo Machi 23,2025.

Papa alishambuliwa haswa na homa ya mapafu, ambayo ni maambukizi ya ambayo yanaweza kusababishwa na bakteria, virusi au fangasi, baada ya kuondolewa sehemu ya mapafu akiwa kijana.

 Mwaka 2013 Francis alikuwa Papa wa kwanza kutoka Amerika na kutoka Ulimwengu wa Kusini. Alimrithi Benedict XVI, ambaye alifariki mwaka 2022. Benedict XVI alikuwa Papa wa kwanza kustaafu kwa hiari baada ya takribani miaka 600.

Papa Francis jina lake kamili ni Jorge Mario Bergoglio, alikuwa Kardinali wa Argentina, na alikuwa na umri wa miaka 70 alipokuwa Papa mwaka 2013.

Bergoglio aliwavutia wahafidhina juu ya mtazamo wake kwa masuala ya mahusiano, huku akiwavutia wanamageuzi kwa msimamo wake wa kiliberali juu ya haki za kijamii.

Lakini ndani ya urasimu wa Vatikani baadhi ya majaribio ya Francis ya kuleta mageuzi yalikumbana na upinzani, lakini alibaki kuwa maarufu miongoni mwa wanamapokeo.

Comments

Popular posts from this blog

BREAKING NEWS: MKURUGENZI WA TANESCO AFARIKI BUNDA KWA AJALI

MIAKA 30 JELA NGUNO WA KWIMBA KWA KUMBAKA KIZIWI

TANZANIA YAISHUKURU ITALIA KUHUSU SGR