VYAMA VILIVYORIDHIA NA KUSAINI KANUNI ZA MAADILI YA UCHAGUZI
Vyama vipatavyo 18 vya Siasa vimeridhia kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa mwaka 2025, hivyo kupata sifa ya kushiriki kwenye uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu Pamoja na chaguzi nyingine zote ndogo zitakazofanyika ndani ya miaka mitano ijayo.
Haya yamebainishwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhan Kailima, na kwamba vyama vya siasa 18 kati ya 19 ndivyo vimesaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi 2025 na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hakijasaini.
"Maadili ya uchaguzi ni muhimu katika kuwezesha uchaguzi huru na haki, na ni muhimu kwa pande zote kuhusika na kusaini maadili hayo, mchakato wa maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani" Amesema Kailima.
Vyama 18 vilivyoridhia kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi 2025, ni ACT WAZALENDO, AAFP,ADA-TADEA, ADC, CCK, CCM, CHAUMA, CUF, MAKINI, DP, NCCR-Mageuzi, NLD, NRA, SAU, TLP, UDP, UPDP na UMD.

Comments
Post a Comment