MAAMUZI YA WAASI WA M23 LEO NCHINI QATAR
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kundi la waasi la M23 wanatazamiwa kufanya mazungumzo yao ya kwanza ya moja kwa moja leo Tarehe 09 Aprili, 2025 mjini Doha nchini Qatar.
Hii inaonesha hatua iliyopigwa kuelekea juhudi za kumaliza moja ya migogoro mikali zaidi katika Afrika ya Kati.
Siku moja baada ya M23 kujiondoa kwa mazungumzo ya amani, Tarehe 18 mwezi Machi Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Felix Tshisekedi, na Paul Kagame Rais wa Rwanda, walikutana nchini Qatar kwa mazungumzo yao ya kwanza ya ana kwa ana mpatanishi mkuu akiwa ni Amir wa Qatar.
Haya yanajiri baada ya Angola kujiondoa kama mpatanishi mkuu wa mzozo kati ya Kongo na M23.
Mzozo wa mashariki mwa Kongo umedumu kwa muda sasa, madini yakitajwa kama kichochea kikubwa, Mzozo umeongezeka haraka tangu Januari 2025, na Maelfu ya watu waliuawa na mamia wakalazimika kuyakimbia makazi yao.

Comments
Post a Comment