KUNDI LA FISI WAVAMIA FAMILIA
Kutokea mtaawa Mahina kata ya Somanda Bariadi mkoani Simiyu Fisi wameua kondoo 21 huku wengine hawajulikani waliopo.
Akielezea kutokea kwa tukio hilo Bwana Mageni Maduhu majira ya saa tano usiku nyumbani kwake ambapo amesema kuwa alisikia kundi la Fisi wakilia nje ya nyumba yake alipoamua kutoka nje na kuwakuta kondoo huku fisi wakakimbia baada ya kumuona.
Aidha Bw. Maduhu ameongeza kuwa alianza kuwafukuza na kukutana na fisi wengine wengi, hivyo akaamua kurudi na alipoangalia kwenye Zizi la kondoo akakuta kondoo 21 wamekufa, huku tisa wakiwa hawaonekani walipo.

Comments
Post a Comment